UTEUZI
Uteuzi wa tuzo hizo hufanywa na raia kupitia tovuti ya Africans Rising (africansrising.org). ). Baada ya uteuzi, wateule watahakikiwa na jopo teule la majaji, kisha wagombeaji wachache wataorodheshwa kama wateuliwa bora zaidi. Kwa kila kategoria (Mwanaharakati Bora wa Mwaka, Harakati Bora ya Mwaka na Mwanaharakati Bora wa Kisanaa wa Mwaka), wateule wawili bora zaidi watachaguliwa kuwakilisha Afrika Kaskazini, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi, Kusini mwa Afrika, na wanadiaspora, kwa jumla ya wateule 36.
Watakaorodheshwa kama wateule bora zaidi wataarifiwa kwa barua pepe au WhatsApp. Wateule hao wataombwa kuwasilisha picha, wasifu, na video (kwa hiari) ili kuonyesha kazi zao. Habari hizo zitawekwa kwenye tovuti ya Africans Rising ili wanachama wetu wapate kujifunza zaidi kuhusu wateule, pamoja na uharakati zao wanapoamua ni nani wa kumpigia kura kama chaguo lao kuu wakati wa duru ya mwisho ya upigaji kura.