[vc_row][vc_column][vc_column_text]Mwongozo wa kupiga kura kwa mujibu wa chaguzi za kamati kuu ya vugu vugu/harakati la Africans Rising unaeleza kwa undani ama kufafanua kuhusu jukwaa la kupiga kura/mtandao wa kupiga kura na mchakato wa kuchagliwa kwa wanachama wapya wa baraza linaloongoza  harakati.Tafadhali pitia maswali na majibu yafuatayo  kisha unaweza kuendelea hadi katika ukurasa wa kupiga kura ambapo unaweza kupiga kura yako katika uchaguzi.[/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][/vc_column][/vc_row][vc_row][vc_column][vcmp_heading vcmp_heading_text=”Chaguzi za kamati kuu ya harakati/vugu vugu la Africans Rising sasa zimefunguliwa! Hivyo inamaanisha nini?”][vc_column_text]Kamati kuu ama bodi simamizi la Africans Rising linasimamia uangalizi wa utendakazi, uratibu na utekelezaji wa mikakati, mipango, pamoja na shughuli za harakati zetu. Katika kipindi cha chaguzi hizi, wewe kama mwanachama wa Africans Rising, unaweza piga kura kuwachagua wanachama saba wapya watakaojiunga na bodi letu. 

Kwa mujibu wa hali ya uwakilishi wa wagombea sita watakaopata idadi kubwa zaidi ya kura katika maeneo yao, mgombea mmoja wa ziada (1) kutoka  kikundi cha walio wachache atachaguliwa kuhakikisha usawa kwenye CC.Hivyo inamaanisha kuwa ikiwa kuna upungufu  wa uwakilishi wa watu wenye ulemavu, watu walio chini ya umri wa miaka 35, au watu kutoka jinsia fulani (kulingana na muundo wa bodi simamizi), basi mgombeaji kutoka kikundi hiki cha wachache anayepokea idadi kubwa zaidi ya kura atachaguliwa kwenye bodi. Wagombeaji katika kategoria hizi wanaweza tambulika kutokana na wasifu wao. 

Kwa jumla, wanachama saba wapya watajiunga na wanachama wetu wanne wanaohudumu katika CC kwa sasa, hivyo basi kufikisha kumi na moja, idadi ya wanachama wa bodi simamizi. [/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][/vc_column][/vc_row][vc_row][vc_column][vcmp_heading vcmp_heading_text=”Kiswahili-Je, ni wapi unaweza kupiga kura?”][vc_column_text]Tumeliunda jukwaa la kupigia kura mtandaoni, lililopachikwa kwenye wavuti la Africans Rising, inayofikiwa kupitia www.africansrising.org/vote. Kwenye ukurasa huu utapata muhtasari wa wagombea wote, pamoja na  mabango yao ya kampeni uliyopangwa kwa mujibu wa maeneo yao katika bara la Afrika: Afrika Kaskazini, Afrika Magharibi, Afrika ya Kati, Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, pamoja na Ughaibuni.

Ukurasa huo ulianikwa mtandaoni kabla ya tarehe tano, mwezi wa Aprili ili wanachama wetu waweze kuwatazama wagombea uchaguzi, lakini bado upigaji kura haukuwa umeruhusiwa. Hivyo basi,wanachama wote wataweza kupiga kura, jukwaa la kupigia  kura litakapopeperushwa moja kwa moja mtandaoni, mnamo usiku wa manane, tarehe tano, mwezi wa Aprili. Basi, lazima kura zote ziwe zimepigwa kabla ya kufungwa kwa jukwaa la kupigia kura, mnamo tarehe kumi na nane, mwezi wa Aprili, saa tano na dakika hamsini na tisa za usiku (All votes must be cast before the close of the voting platform on April 18 at 11:59 PM GMT). [/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][/vc_column][/vc_row][vc_row][vc_column][vcmp_heading vcmp_heading_text=”Kiswahili-Je, Jukwaa la kupiga kura lafanya kazi kwa njia ngani?”][vc_column_text]Mtandao wa kupigia kura/Jukwaa la kupigia kura litakuuliza nambari ya OTP inayokuruhusu / kukupa idhini ya kupiga kura.Kupitia chaguzi zilizotolewa, basi utachagua kupokea nambari ya OTP kupitia barua pepe au SMS kulingana na matakwa yako(unastahili  kuchagua kutoka kwa chaguzi zilizotolewa kwenye wavuti). Baada ya kupokea OTP, utabonyeza/utajaza nambari kwenye nafasi ufaao, kisha jukwaa litakuwezesha kuwapigia kura wagombea sita  wa chaguo lako, mmoja kutoka kila eneo.Ili kukamilisha kura yako, basi lazima uchague mgombea mmoja kwa kila mkoa.(Kwa mfano: Mfumo huo wa kupiga kura  hautakuruhusu kuwasilisha kura kwa mgombea mmoja katika mikoa minne tu). Kura zote ziwe zimepigwa kabla ya kufungwa kwa jukwaa la kupigia kura, mnamo tarehe kumi na nane, mwezi wa Aprili, saa tano na dakika hamsini na tisa za usiku. (All votes must be cast before the close of the voting platform on April 18 at 11:59 PM GMT). 

Ukiwa na changamoto yoyote kuhusiana na awamu hii ya mchakato wa kupiga kura, tafadhali wasiliana na: ccelection@africans-rising.org [/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][/vc_column][/vc_row][vc_row][vc_column][vcmp_heading vcmp_heading_text=”Kiswahili-Nani anastahili kupiga kura katika chaguzi za bodi simamizi/kamati kuu?”][vc_column_text]Ili uweze kupiga kura yako katika chaguzi za kamati kuu/ bodi simamizi, lazima uwe tayari ushasajiliwa kama mwanachama. Hivyo, wanachama wa Africans Rising waliojisajili mnamo au kabla  tarehe Moja, Machi, basi wako huru kupiga kura katika chaguzi za bodi simamizi/kamati kuu, za  mwaka huu. Katika kampeni hizi, kila mwanachama binafsi atakuwa na alama moja (1) ya kura na kila mwanachama wa kishirika(anayewakilisha zaidi ya mtu mmoja) atakuwa na alama mbili (2) za kura katika chaguzi hizo. Kategoria hizi/vikundi hivi, vya wanachama binafsi na wanachama wa kishirika, vilichaguliwa, ama viliamuliwa na mwanachama husika wakati wa usajili wake. 

Kura za kishirika hazitarekodiwa hivyo mara moja kama kura mbili, kutokana na  changamoto za kiufundi zinazohusiana na mfumo wa kupiga kura,lakini kura ya pili itajumlishwa moja kwa moja wakati wa upigaji kura.

Tafadhali endelea kwenye ukurasa wa kupiga kura hapa: https://africansrising.org/vote/[/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][/vc_column][/vc_row]